Africancrops.net | Striga Home
|
Angamiza Striga kwa Kutumia Mahindi ya Ua Kayongo Hybrid! |
|||||||||
|
Striga imeharibu mimea ya nafaka ya wakulima katika mikoa ya Nyanza na Magharibi. Imevamia karibu hekari 200,000 za eneo la ukulima nchini Kenya na matokea yake ni hasara ya karibu Shg. Milioni 800 kila mwaka pamoja na ukosefu wa usalama kivyakula katika magaharibu mwa Kenya. Wakulima nchini Kenya sasa wanao aina mpya ya mahindi iitwayo Ua Kayongo iliyopakwa dawa iitwayo StrigawaTM inayoua Striga. Kimsingi, teknolojia hii huua tete zinazoota za Striga zinapoanza kuvamia mihindi. Kwa wanasayansi, teknolojia hii inaitwa mahindi-yanayohimili ya Imazapyr (Mahindi-IR) au mfumo wa kiwanja wazi. Hii inatokana na dawa ya wadudu asilia inayohimili katika mahindi yaliyotambuliwa kwa mara ya kwanza na watafiti wa BASF, na baadaye ujuzi huo ukajumuishwa katika sampuli za mahindi ya Kenya na wazalishaji wa Kiafrika wa International Maize and Wheat Improvement Centre (CIMMYT) na wale wa Kenya Agricultural Reasearch Institute (KARI). Kwa sasa makampuni matatu ya mbegu, Kenya Seed, Lagrotech na Western Seed yanazalisha mbegu hii ya mahindi kwa ajili ya kufanyiwa majaribio mashambani. Makampuni hayo yameamua kuuza mahindi haya mapya kwa jina la Ua Kayongo H1 (Striga killer). African Agricultural Technology Foundation (AATF) ilianzishwa ili kuwasaidia wakulima kufikia teknolojia mwafaka. Kuanzisha teknolojia ya Mahindi-IR kumepewa Ili kufikia lengo hilo, AATF inashirikiana na CIMMYT, KARI, BASF, Mashirika yasiyokuwa ya serikali (We RATE-FORMAT, SACRED-Africa, SCODP), makampuni ya mbegu, wauzaji (Kenya Seed, Lagrotech, Western Seed), TSBF-CLAT) na wengineo ili kuendesha maonyesho ya mashambani na siku za mafundisho magharibi mwa Kenya. Ua Kayongo H1 hupandwa na kushughulikwa kama mbegu nyingine zozote za mahindi. Hata hivyo, Ua Kayongo imepakwa dawa ya StrigawayTM. Ni muhimu wakulima wanawe mikono yao baada ya kuitumia na kabla ya kushughulikia mazao mengine. Ua Kayongo inaweza kupandwa pamoja na mimea ya familia ya maharagwe, lakini sio katika shimo moja. Ua Kayongo inaweza kujumuishwa na teknolojia nyingine za kuua Striga, kama vile mfumo wa Push-Pull au MBILI ikipandwa pamoja na njugu, dengu ya dhahabu, soya au lablab. Kutumia Ua Kayongo kunapunguza kwekwe unapopalilia mara ya kwanza. Wakati wa msimu ujao wa mvua ya masika wa 2005, mashamba ya maonyesho ya Ua Kayongo katika maeneo yanayokuwa na Striga kwa wingi yataonyesha ufaafgu wake. Ua Kayongo itasambazwa kwa familia zaidi ya 16,000 siku za mafundisho kadhaa zitaendeshwa na warsha itafanywa mnamo Juni 2005.
|